Alichosema MO Dewji baada ya kutembelewa na kocha Simba SC leo


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Simba SC,Mohammed Dewji amefunguka mara baada ya timu hiyo kufuzu kucheza robo fainali ya Klabu bingwa Afrika.

Mo Dewjia amepongeza kikosi hicho na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliofanya, huku
akiwataka mashabiki kuendelea kuwa bega kwa bega na timu hiyo.

"Huu ni ushindi wetu sote! Jana tumeandika historia kuwa klabu pekee Tanzania na Afrika
Mashariki kuingia robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu.

Ameendelea kwa kusema, 'Nawapongeza na kuwashukuru wachezaji, benchi la ufundi,
viongozi, wanachama, mashabiki, na wapenzi wote wa SIMBA!. Safari inaendelea! Tuendeleze
mshikamano wetu ili tufikie lengo letu la kuwa mabingwa wa Afrika, Insha’Allah, asante Kocha
Aussems kwa kunitembelea leo,'.


Comments