Taarifa za usajili barani Ulaya Alhamisi hii, Bale, Hazard, Eriksen, Hudson-Odoi, Thuram na wengine sokoni
Real wanaweza kuitisha dau la £131m ili kumuuza Bale, ambaye anahusishwa na uhamisho wa Manchester United. (TeleMadrid, via Talksport).
Au Real Madrid huenda ikamwachilia mshambuliaji wa Wales Gareth Bale kuondoka mwisho wa msimu huu na watamtumia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kama chambo katika majadiliano ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 28, ama kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27. (Marca)
Manchester United inatarajiwa kumpatia mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 21, mkataba mpya wa miaka sita baada ya mazungumzo kufua dafu. (Daily Mirror)
Paris St-Germain ina mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Uingereza Callum Hudson-Odoi, 18, ambaye pia analengwa na klabu ya Bayern. (Sun)
Mkufunzi wa zamani wa Ufaransa na Paris St-Germain Laurent Blanc atakuwa miongoni mwa warithi wa kocha wa Maurizio Sarri iwapo Chelsea itaamua kumfuta kazi raia huyo wa Itali wiki ijayo.
Kiungo wa kati wa Paraguay Miguel Almiron alikuwa anachunguzwa na Manchester United kabla ya kujiunga na Newcastle, kulingana na ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Newcastle Chronicle)
Tottenham inatumai kupiga hatua muhimu katika ufunguzi wa uwanja wao mpya unaoweza kubeba takriban watu 62,062 msimu huu huku majaribio yakipendekezwa kufanyika tarehe 16 na 23 Machi. (London Evening Standard)
Chelsea na Liverpool inamchunguza kinda wa miaka 17 Khephren Thuram – mtoto wa aliyekuwa mchezaji wa Ufaransa Lilian Thuram. Mchezaji huyo anayeichezea timu ya Ufaransa ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 bado hajatia kandarasi ya kuwa mchezaji wa kulipwa katika klabu ya Monaco. (Daily Mail)
Beki wa Leicester na Croatia Filip Benkovic, 21, amethibitisha lengo lake la kurudi kuichezea timu hiyo msimu ujao baada ya mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Celtic. (Leicester Mercury)
Rais wa La Liga Javier Tebas ni miongoni mwa wanaotaka kumrithi Richard Scudamore kama afisa mkuu mtendaji wa ligi ya Premia nchini Uingereza. (Times)
Mshambuliaji wa Reading na Nigeria Sone Aluko, 30, anakamilisha uhamisho wa kutaka kwenda kuichezea klabu ya China ya Beijing Renhe. (Mail)
AC Milan inamtaka mchezaji anayelengwa na klabu ya Celtic Timothy Castagne baada ya kufurahishwa na mchezo wa beki huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 23 akilipokuwa akiichezea Atalanta katika ligi ya Serie A. (Inside Futbol)
Liverpool inatarajiwa kuzuru Marekani ya kaskazini badala ya bara Asia mwisho wa msimu huu . (Liverpool Echo)

Comments
Post a Comment