Simba SC wanaendelea kuzikusanya point tu ili watetee taji la TPL


Simba SC ambao ndio Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara, leo walikuwa Iringa katika uwanja wa Samora kucheza dhidi ya Lipuli FC ikiwa ni muendelezo wa michezo yao ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2018/2019, Simba ndio timu ambayo ina viporo vingi kwa sasa.

Wakiwa wanajua kuwa wapo nyuma kwa michezo mingi na point pia, Simba dhidi ya Lipuli wamehakikisha wanatoka na point zote tatu kutoka katika uwanja wa Samora kwa kuifunga Lipuli FC kwa magoli 3-1, magoli ya Simba yakifungwa na Clotous Chama dakika ya 6, 44 na Meddie Kagere dakika ya 58.

Lipuli FC waliopo nafasi ya 5 katika msimamo wa Ligi Kuu goli lao pekee lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 18 wakiwa na point 38 walizopata katika michezo yao 28, Simba wanaendelea kuwa nafasi ya tatu licha ya kupunguza viporo vya na sasa wana viporo sita wakiwa na point 48, Yanga akiongoza Ligi kwa kuwa na point 61, wakicheza michezo 25 sawa na Azam waliopo nafasi ya pili wakiwa na point 50.

Comments