Kampuni ya simu ya Samsung imezindua smartphone mpya aina ya Galaxy Fold na 5G Galaxy S10.
Galaxy Fold inatarajiwa kuingia sokoni katika muda wa miezi miwili mapema kuliko vile ilivyotarajiwa.
Galaxy S10 5G inatajwa kuwa moja ya simu kubwa ambayo imewahi kutengenezwa na kampuni ya Samsung na inakuja na progamu za kusifika.
Kampuni ya Samsung inasema kuwa Galaxy Fold inauwezo wa kufunguka kwa hadi inchi 7.3 (18.5cm) na kuendesha apps tatu kwa wakati mmoja.
Galaxy Fold inauwezo wa kufunguka kwa hadi inchi 7.3 (18.5cm) na kuendesha apps tatu kwa wakati mmoja.
Samsung imeongeza kuwa programu za Whatsapp, Facebook, YouTube na Microsoft Office zitasawazishwa ili kufanya kazi kwa ubora zaidi katika simu hii mpya.
Imesema kuwa wameunda mfumo mpya ambao unafanya kazi ya kuhimili maelfu ya kurasa zitakazo kunjwa bila kuathiri utenda kazi wa simu yenyewe.
Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia nchini Korea Kusini imesema simu hiyo ina kamera sita- tatu za nyuma three, mbili za upande na moja ya mbele- kuhakikisha inaweza kupiga picha bila kujali imeshikiliwa vipi.
Mfumo wa 4G wa Galaxy Fold unatarajiwa kuwa madukani kuanzia Aprili 26 na itauzwa kwa bei ya dola 1,980 (£1,515).
Samsung imeielezea simu hii mpya kama kifaa cha ''kifahari''
"Fold itawapatia watumiaji wake thamani ya technolojia mpya hasa wale wanaopenda simu zilizo na skrini kubwa bila kuharibu ubora wake," alisema Carolina Milanesi mmoja wa washauri wa masuala ya ubunifu wa teknolojia.
Simu hii inapatikana kwa rangi nne
Simu hii imepokelewaje?
Baadhi ya wadadisi wa masuala ya teknolojia wanatilia shaka uwezo wa simu hiyo mpya.
"Kinadharia simu hii inavutia sana: zina uwezo wa kupunguza skrini kubwa kuwa ndogon," alisema Neil Mawston afisa kutoka kampuni ya utafiti ya Strategy Analytics.
"Lakini ukweli wa mambo ni kuwa wateja hawana uhakika wa jinsi itakavyofanya kazi, na programu zake bado hazijaimarishwa vilivyo'
Comments
Post a Comment