Rais mstaafu Jakaya Kikwete na aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa walivyowasili kwenye msiba wa Ruge

Ikiwa ni siku ya pili tangu Tanzania iondokewe na mtu muhimu sana, Viongozi mbalimbali wa Serikali wameendelea kuhudhuria nyumbani kwa wazazi wake marehemu Ruge Mutahaba ambaye amefariki dunia akiwa anapokea matibabu nchini Afrika ya Kusini.


Na leo wameweza kuhudhuria baadhi ya viongozi wastaafu wakiongozwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mke wake lakini pia aliyekuwa Waziri mstaafu Edward Ngoyai Lowasa.
Image result for picha za matukio ya msiba wa ruge mutahaba
Rais wa Awamu ya Nne Dkt Jakaya Kikwete akitia saini daftari la waombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini,Pichani
kushoto ni Mke wa Rais Mstaafu Salma Kikwete na
kulia ni
Naibu Waziri wa Habari
, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza
Image result for picha za matukio ya msiba wa ruge mutahaba
Juliana Shonza na Rais Dkt Jakaya Kikwete akiingia katika Msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini.

Baadhi ya wabunge na viongozi wa kisiasa waliofika siku ya leo katika Msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini.



Baadhi ya vijana wa THT wakiimba wimbo wa uombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini

Picha ya vijana wa THT wakiimba wimbo wa uombolezaji katika msiba wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi wa Clouds Ruge Mutahaba aliyefariki Nchini Afrika Kusini.

Comments