Ikiwa ni siku ya huzuni kwa Watanzania baada ya kuondokewa na mtu muhimu sana katika sekta ya burudani ambaye alikuwa msaaka vijana wengi sana pia akiibua vipaji vya vijana mbalimbali na kuvikuuza, huyu sio mwingine bali ni Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds media Group, Bwana Ruge Mutahaba ambaye mpaka sasa ni marehemu baada ya kupoteza maisha akiwa kwenye matibabu nchini Afrika ya kusini.
Ratiba ya awali ya mazishi ya Ruge na mahali atakapozikwa yawekwa wazi
Mwili wa marehemu Ruge Mutahaba utakuja kesho hapa nchini na kufika nyumbani kwa wazazi wa marehemu pale mikocheni nyuma ya shule ya feza .Watanzania watamwaaga mwili wa marehemu siku ya jumamosi, na mwili utasafirishwa siku ya jumapili kuelekea mkoa wa Bukoba kwa taratibu za mazishi.Na siku ya jumatatu mwili utazikwa mkoani Bukoba.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe katika msiba wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole kwenye msiba wa Ruge Mutahaba.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefika nyumbani kwa familia ya Ruge Mutahaba na kutoa pole za msiba ambapo pia ameweza kumwelezea marehemu Ruge Mutahaba.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba wakati alipokwanda nyumbani kwao marehemu.
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Taifa limepoteza kijana aliyekuwa msatari wa mbele kuwahamasisha vijana wajitambue wawe wazalendo kwa nchi yao.
Waziri Mkuu, Makonda wawasili kwa wazazi wa marehemu Ruge
(Pichai ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na baba mzazi wa marehemu Ruge Mutahaba wakati alipokwanda nyumbani kwao marehemu.
Baadhi ya waombolezaji. Watu mbalimbali wakiwa katika msiba wa Ruge Mutahaba. Waombolezaji.
Comments
Post a Comment