Nyuki mkubwa duniani agundulika

Nyuki mkubwa zaidi duniani
Wanasayansi wanasema kwamba wamegundua uwepo wa kile kinachoaminika kuwa nyuki wakubwa zaidi duniani nchini Indonesia.

Nyuki huyo mwenye ukubwa wa kidole gumba na mabawa yenye upana wa sentimita 6, hapo awali ilidhaniwa kuwa wameangamia kabisa.

Amepewa jina la Wallace, linalotokana na mtaalamu wa viumbe Alfred Russel Wallace, aliyevumbua mdudu huyo mwaka 1858.

Mtafiti wa sasa ambaye amempiga picha nyuki huyo, amesema ndoto yake ni kufanya aina hiyo ya nyuki kama nembo ya uhifadhi wa mazingira.

Wanasayansi pia wamepata viumbe kadhaa ambao walipotea duniani tangu mwaka 1981.

Mwezi Januari mwaka huu wanasayansi hao walifuata nyao za Wallace katika ziara ya Indonesia katika juhudi za kupata picha ya nyuki huyo.

Eli Wyman akiwa na sampuli ya nyuki mkubwa zaidi
Eli Wyman akiwa na sampuli ya nyuki mkubwa zaidi

"Inafurahisha sana kuona nyuki mkubwa hivi ambaye tulidhania hayuko duniani," alisema mpiga picha wa Clay Bolt, ambaye alipiga picha ya kwanza ya nyuki huyo.

Sifa za nyuki mkubwa zaidi duniani
ukubwa wa kidole gumba na mabawa yenye upana wa sentimita sita.
Anatengeneza makaazi yake kutokana na majani ya magamba ya miti.
Nyuki huyo anakula mchwa wanaopatikana kwenye miti.
Wallace, aliyevumbua nyuki huyo kwa alisema"ana umbo kubwa zaidi ya wadudu wengine wanaopatikana kwenye spishi hiyo".

Uvumbuzi huu umefufua matumaini kuwa misitu inayopatikana katika visiwa vya Moluccas kaskazini, nchini Indonesia huenda ina aina za wadudu wakipekee duniani.

Kwa sasa hakuna sheria zozote zinazodhibiti shughuli za kibinadamu katika misitu hiyo.

Eli Wyman, mmoja wa watafiti kutoka chuo kikuu cha Princeton, amesema kuwa ana matumaini uvumbuzi huu utawapa motisha wa kufanya utafiti zaidi kuhusiana na historia ya nyuki katika juhudi za kuhakikisha mdudu huyo hataangamizwa duniani.

Comments