Nguli wa Series ya Empire Jamal, aachiwa kwa dhamana kutokana na kuidanganya Polisi, Trump atia neno kwenye sakata lake
Kama unaikumbuka series ya Empire iliyojizolea umaarufu kutokana na waigizaji husika walioshiriki katika series hiyo, Ikumbwe hii ni moja ya series ambayo imeangaliwa sana na kuwapa heshima wakubwa washiriki wa series hiyo.
Mmoja wa waigizaji wa Empire Jussie Smollett ameachiwa kwa dhamana kufuatia kushikiliwa na polisi kwa masaa kadhaa na kisha kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya kuidanganya polisi.
Smollett amekana mashtaka yote, ameachiwa kwa dhamana ya $100k pia amekabidhi hati yake ya kusafiria. Polisi wamezungumza kuwa Smollett alifanya kitendo hicho cha kupanga shambulio kutokana kutoridhishwa na malipo anayolipwa kwenye Empire, hivyo akaona bora atafute ukubwa wa jina lake kwa kudanganya umma kuwa amefanyiwa vitendo vya kibaguzi.
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa maoni yake pia kwenye sakata hili, ameandika kupitia twitter kuwa: “Vipi kuhusu maneno yako machafu juu ya kauli ya ‘MAGA’ na mamilioni ya watu uliowaaminisha kuwa ulitukanwa na kufanyiwa ubaguzi wa rangi?”
Baadaye Smollett alitembelea eneo inapofanyika utengenezaji wa tamthilia ya Empire na kuwaomba radhi wote kwa kusema hakufanya hivyo:
“I’m sorry I’ve put you all through this and not answered any calls. I wanted to say I’m sorry and, you know me, I would never do this to any of you, you are my family. I swear to God, I did not do this.”

Comments
Post a Comment