Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nandy ameshindwa kujizuia mbele ya kamera za Clouds TV kwenye kipindi cha Clouds 360 na kutoa machozi juu ya taarifa za kuugua kwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Groups, Ruge Mutahaba.
Nandy alianza kuelezea namna alivyomfahamu hadi kukutana na Ruge Mtahaba “Ruge amenifanyia vitu vingi ni mtu ambaye anashika nafasi nyingi sana kwenye maisha yangu anasimama kama Baba, kaka, Boss ana maana kubwa sana kwangu sio kimuziki hata maisha yangu binafsi, mimi mpaka kuwa hapa yeye anamchango mkubwa sana kuanzia kuijenga brand yangu“
Nandy amesema kuingia kwake THT alisaidiwa na Ruge, hii ni baada ya kutoka kwenye shindano la Tecno Own The Stage nchini Nigeria.
Amedai kuwa siku ya kwanza kukutana naye, alimpa CD za kazi yake lakini Ruge alizivunja mbele yake na kumshauri ajiunge na THT apigwe msasa.
Kwa upande, mwingine Nandy amesema atajitolea kuchanga pesa kadri awezavyo kusaidia matibabu ya Ruge Mutahaba.

Comments
Post a Comment