Mo Dewji ashindwa kujizuia baada ya Simba kuwashushia kipigo waoka mikate Azam FC ‘Kwetu raha tu’

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba hii leo wameibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3 – 1 dhidi ya klabu ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kuu uliyopigwa uwanja wa Taifa.

Mara baada ya miamba hiyo ya soka kupata ushindi huo, mfanyabiashara maarufu nchini na muwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji ameonyesha kufurahishwa na matokeo hayo hali iliyopelekea hadi kuandika jumbe kwenye akaunti zake za kijamii za Twitter na Instagram unaonyesha furaha yake.

Waliyotupia mabao hayo ni John Bocco pamoja na Meddie Kagere aliyefunga mawili huku bao pekee la Azam likifungwa na Frank Domayo dakika za lala salama.



Comments