Maurizio Sarri alivyojibu kwa nini Kante hamchezeshi nafasi aliyozoeleka


Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea club ya Chelsea Ng’olo Kante kuwa hana furaha katika club hiyo kocha wake Maurizio Sarri amefunguka kuhusiana na kichodaiwa kumnyima raha Kante.

Kante iloripotiwa kuwa hana furaha katika club hiyo akiwa chini ya Kocha Maurizio Sarribkwa sababu hampangi nafasi aliyozoea kuicheza ya kiungo mkabaji, hivyo kocha Sarri ameeleza kwa nini hampangi Kante kama (holding midfielder) kama ilivyokuwa imezoeleka.

“Watu wengi wanasema kuwa unakaidi kumchezesha N’golo Kante nafasi ambayo alikuwa anacheza akiwa na Ufaransa na Chelsea kabla ya ujio wako”>>>Mwandishi

“Inategemea na namna mpira unavyouona katika hiyo nafasi unayoitaka awe unatakiwa kuuamisha mpira kwa haraka sana na hiyo sio moja kati ya sifa za N’golo, N’golo ana matumizi na sisi lakini kwa hili sio moja kati ya sifa za ubora wake”>>>Maurizio Sarri

“Ameshinda World Cup na mataji mawili ya Ligi Kuu England?”>>>Mwandishi

“Lakini hiyo ni kwa mfumo mwingine”>>> Maurizio Sarri

Kama utakuwa unakumbuka vizuri kocha Maurizio Sarri ambaye anahusishwa nafasi yake kuwa mashakani kwa timu hiyo kuwa katika mwenendo mbovu, alijiunga na Chelsea July 2018 akitokea club ya Napoli ya Italia na sasa nafasi yake anahusishwa kwa karibu kutaka kumchukua kocha Zinedine Zidane ndio awe mrithi wake.


Comments