Marufuku Fifa: Klabu ya Chelsea imesema itakata rufaa kupinga uamuzi wa Fifa dhidi yake

Bertrand Traore akishikilia jezi ya Chelsea mbaada ya kusajiliwa mwaka 2014
Bertrand Traore

Chelsea imepigwa marufuku ya kuwasajili wachezaji kwa miaka miwili baada ya kukiuka kanuni ya kuwasajili wachezaji wadogo, Fifa imetangaza.

Marufuku hiyo itakayodumu hadi mwaka 2020, haitajumuisha kuwazuilia wachezaji kuhama klabu hiyo na pia haijumuishi timu ya wananawake.

Klabu hiyo inayoshiriki ligi ya Primia imesema itakata rufaa kupinga uamuzi huo.

Chelsea pia imepigwa faini ya euro £460,000, huku Shirikisho la soka nchini Uingereza (FA) ikiwatoza faini ya euro £390,000.

Uamuzi huo unafuatia uchunguzi wa Fifa kuhusu Chelsea inavyowasajili wachezaji wa chini ya miaka 18, ikiwa ni pamoja na usajili wa mashambuliaji wa zamani Bertrand Traore.

Shirikisho hilo la dunia linalosimamia mchezo wa kandanda linasema kuwa Chelsea imevunja sheria katika usajili wa wachezaji 29 kati ya 92 waliyochunguzwa.

"Tunakubaliana na Fifa kwa kuafiki kuwa hatukuvunja sheria kuhusiana na visa 63 vya usajili wa wachezaji hao, lakini klabu hii imeshangazwa na hatua ya Fifa kukataa maelezo kuhusiana na wachezaji 29 waliyosalia," inasema taarifa ya kutoka Stamford Bridge.
A Chelsea flag
"Chelsea imezingatia kanuni zote na inajiandaa kuwasilisha rufaa yake kwa Fifa."

Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeagizwa na Fifa "iingilia kati" suala la usajili na uhamisho wa wachezaji wadogo katika vilabu vya soka.

Msemaji wa shirikisho hilo amesema kuwa litazingatia agizo hilo"kikamilifu" lakini "linahoji" mfumo wa kitoa adhabu wa Fifa.

Taarifa hiyo pia inasema: "FA inapania kukata rufaa dhi ya uamuzi huo. Hata hivyo tutaendelea kushirikiana na Fifa na Chelsea ili kusuluhisha masuala yaliyoibuka katika kesi hii."

Kulingana na ufichuzi wa Football Leaks, mtandao wa Ufaransa wa Mediapart ulidai kuwa mwezi Novemba usajili wa Chelsea wa wachezaji 19 ulichunguzwa katika uchunguzi huo wa miaka mitatu.

Mediapart inadai kuwa wachezaji 14 waliyosajiliwa walikuwa chini ya miaka 18.

Mara ya kwanza kuripotiwa kuwa Chelsea inachunguzwa ilikwa Septemba mwaka 2017.

Mchezaji wa kimataifa wa Burkino Faso Bertrand Traore - ambaye sasa anachezea klabu ya Lyon inayoshiriki Ligue 1 - alitia saini mkataba wa Chelsea mwaka 2013 akiwa na miaka 18 lakini hakusajiliwa hadi mwezi Januari mwaka 2014.

Mediapart inaripoti kuwa Fifa ina ushahidi kuwa Chelsea ilidanganya kuhusina na tarehe ya usajili huo, baada ya kubaini kuwa Traore aliichezea The Blues mara 25 licha ya kwamba hakua amesajiliwa na shirikisho la soka nchini Ungereza FA.

Chelsea imekiri kuwa ilimlipa mama yake euro £155,000, ikiwa ni pamoja na £13,000 walizomlipia- AJE Bobo-Dioulasso - mwezi Aprili mwaka 2011 kukubali awatilie saini mkataba

Mkataba huo inadaiwa kufikiwa miaka minne na nusu licha ya kuwa ya kuwa sheria inayodhibiti usajili wa wachezaji waliyo chini ya miaka 18 ni miaka mitatu.

Chelsea inadai kuwa ilimlipiaTraore euro £20,000-kwa mwaka kusomea shule ya Whitgift mjini Surrey.

Real Madrid na Atletico Madrid zilipigwa marufuku ya usajili baada ya kupatikana na hatia ya kuwasajili wachezaji wadogo mwaka 2016.

Klabu ya Barcelona pia ulipewa marufuku ya miezi 14 baada ya kukiuka kanuni ya usajili wa wachezaji wa kimataifa waliyo chini ya miaka18 mwaka 2014.

Hatahivyo rufaa iliyowasilishwa na Barcelona iliwapunguzia adhabu ya mwaka mmoja katika hatua iliyowawezesha kuwasajili Luis Suarez, Ivan Rakitic, Jeremy Mathieu, Claudio Bravo na Marc-Andre ter Stegen.

Sheria za Fifa zinasemaje?

Fifa inapiga marufuku usajili wa wachezaji waliyo chini ya miaka 18 katika mataifa tofauti hadi wafikia masharti fulani muhimu

Ilibuni sheria hizo ili kuwalinda watoto na kuwakinga dhidi ya walanguzi ambao huenda wakawatumia vibaya kwa maslahi yao.

Wachezaji waliyo chini ya miaka 18 wanaweza kuhamia ughaibuni ikiwa:

Wazazi wao wamehamia taifa ambalo ni nyumbni kwa klabu yake mpya na wawe wamehama kwa sababu ambazo hazihusiani na kandanda.
Vilabu vyote viwe chini ya mataifa ya muungano wa ulaya na mchezaji wawe na umri wa kati ya miaka 16 and 18.
Klabu inayowanunua wachezaji hao pia lazima ifikie vigezo vya sheria ya kuwasomesha, kugharamia mazoezi na maisha yao kwa ujumla.
Wachezaji waishi katika eneo la 100km na ilipo klabu husika.

Comments