Clab ya Singida United imefanikiwa kumpelekaa mchezaji John Tibar George katika Club ya Mfk FC iliyopo Jamhuri ya Czech, Tibar anaondoka ameondoka usiku wa jana akipitia Ufaransa ambako atakaa kwa muda usiopungua wiki moja kwenye Club Toulouse FC kwa ajili ya Fitness na Techniques.
Vibali vyote vimeshatumwa kwenye club yake mpya ikwepo ITC, hivyo anakwenda huko kuanza maisha ya soka moja kwa moja, uongozi wa Singida United unashukuru sana wote waliohusika kufanikisha hili, zaidi TFF kwa ushirikiano wao wote katika kipindi chote cha kuhakikisha vibali vya mchezaji huyu vinapatikana kwa wakati.
Timu ya Mfk ni timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Czech hivyo itakuwa msaada kwa taifa la Tanzania kwa kuendeleza kipaji cha mchezaji kwenda kucheza soka katika nchi zilizoendelea, hata hivyo kupata kwake nafasi ya kufanya mazoezi na Toulouse FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Ufaransa ni fursa pia kwake kujifunza mengi.
Comments
Post a Comment