Mshambuliaji wa zamani wa club ya Man United anayekipiga katika club ya LA Galaxy ya Marekani kwa sasa Zlatan Ibrahimovic, amezisikia taarifa za kukosolewa kwake na baadhi ya watu hususani wanaombeza na kumuita mzee katika soka kwa sasa, Zlatan amesikia kejeli hizo na kuzitolea kauli kwa wanaobeza kutokana na umri wake.
Zlatan mwenye umri wa miaka 37 ameamua kuvunja ukimya na kuahidi kuwa kwa wale wanaomsema mzee katika soka, atahakikisha akiwa katika Ligi Kuu ya Marekani MLS, atavunja kila rekodi ili kudhiirisha kuwa umri wake wa miaka 37 kuwa sio tatizo katika kuonesha kipaji chake cha soka.
Staa huyo wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya Sweden ambaye amewahi kujilinganisha na mvinyo kutokana na kuwa bora kila umri wake unavyozidi kuwa mkubwa, akihojiwa na CNN amenukuliwa akisema “Kwa sababu wanasema mimi ni mzee nitahakikisha navunja kila rekodi iliyokuwa imewekwa MLS”
Zlatan Ibrahimovic kabla ya kujiunga na LA Galaxy akitokea Man United mchezaji huru aliwahi kuvichezea vilabu mbalimbali kama Malmo ya kwao Sweden Ajax ya Uholanzi, Juventus, Inter Milan, AC Milan ambazo zote za Italia pamoja na FC Barcelona ya Hispania.
Comments
Post a Comment