Maandalizi ya kumzika marehemu Ruge Mutahaba katika kijiji cha Kiziru Wilaya ya Bukoba yamepamba moto na ujenzi wa kaburi umeanza leo.
Siperatus Mbeikya ambaye ni mmoja wa wanafamilia amesema taratibu zinaendelea ikiwa ni pamoja na kupokea wageni kutokana maeneo mbalimbali.
Pia, amesema maandalizi hayo yamekwenda sambamba na kukubaliana na kikosi cha usalama barabarani sehemu utakapopita msafara wenye mwili wa marehemu Ruge.
Pilikapilika zimeongezeka katika eneo la msiba ikiwa ni pamoja na kumwaga vifusi kwenye maeneo korofi.
Marehemu Ruge anatarajiwa kuzikwa Jumatatu, wakati mwili wake utawasili Dar es Salaam kesho Ijumaa na kuagwa Jumamosi.
Comments
Post a Comment