Mwanadada Kimnana ambae amewahi kuwa video vixen katika baadhi ya nyimbo za wasanii hapa nchini amefunguka na kusema kuwa katika kazi hiyo kwa sasa imekuwa hailipi na wala pesa yake haikidhi mahitaji ya maisha na brand ya video Vixen.
Kimnana anasema kuwa watu wengi wamekuwa wakiwachukua katika video na kuwalia pesa kidogo bila kujali kuwa kazi zao zinaweza kuuzia sana kuliko hata pesa wanayolipwa katika kufanya kazi hiyo.
Hata hivyo mwanadada huyo anasema kuwa kwa sasa kama kuna mtu anataka kufanya nae kazi basi dau lake la chini ni shilingi milioni moja na kama haipo basi ni bora kuacha kufanya kazi hiyo.
kazi hiyo kwa sasa sigfanyi kwa sababu hailipi, kwa sababu hailipi kabisa, uklipwa sana basi shilingi laki tano hivyo mimi kufanya kazi hiyo chii ya milioi moja sifanyi.
Kimnana amepata umaarufu sana hapa kipindi cha nyuma kutokana na kuwa na mahusiano na msanii diamond platinumz.
Comments
Post a Comment