Msanii Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa moja ya kitu anachokilingia sana kwa mwanamke wake huyo mpya ambae anatarajia kumuoa hivi karibuni ni kwamba mwanamke huo anajua sana kupika na amekuwa akimuweka sawa karibia kwa kila kitu.
Diamond anasema kuwa watu wasishangae sana kunenenpa kwake ni kutoaka na mapishi na vyakula vya mwanadada huyo ambae amekuwa akimpikia kila siku na pia hata style zake za nywele kwa sasa zimekuwa zikitengenezwa na mke wake huyo.
Mapishi shemeji yenu anajua sana, matunzo moyo umetulia sana, nadekezwa , natengenezwa styke za nywele, yeye ndio anasema baby nyoa hivi , baby tengeneza hivi , mwanamke anatakiwa awe kama christian ronaldo anapiga mpita kwa miguu yote.
Kwa kuongezea swala hilo, Diamond anaongezea na kusema kuwa amekuwa akimpenda mwanamke huyo kwa sababu hataki makuu na mtu na hapendi kulinga wala mambo ya kishari na kujibizana na watu au kusema watu vibaya.
Comments
Post a Comment