Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis ataondoka rasmi kazini mwezi Februari mwakani
Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis, amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa utawala wa Bwana Donald Trump.
Bwana Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twitter, akisema kuwa Jenerali huyo atastaafu "Kwa heshima na taadhima" mwishoni mwa mwezi Februari mwaka ujao.
Hilo linatukia siku moja tu baada ya tangazo la Rais lililosababisha utata mkubwa, kwamba Marekani imeamua kuyaondoa majeshi yake kutoka Syria.
Kwenye barua yake, Jenerali Mattis, kwa uzito mkubwa, aligusia kiini cha kujiuzulu kwake kwamba kumesababishwa na tofaurti za sera aliyo nayo na ile ya Bw Trump.
Idadi kubwa ya wanachama wakuu wa chama chake Trump cha Republican, wamelichukulia swala hilo kujiuzulu kwa Jenerali Mattis kwa uzito mkubwa.
Kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Seneti, Mitch McConnell amesema kwamba, "ana huzuni kubwa" kwa kuondoka kwa Mattis kwa sababu ya "kutofautiana" kati ya Jenerali Mattis na Rais.
Wanajeshi wa Marekani waliingia Syria mwaka 2015
Bwana Trump hajamtaja mtu kuchukua mahala pake, lakini amesema atafanya hivyo muda mfupi ujao.
Kuondoka kwa waziri huyo wa ulinzi ni hatua ya hivi punde zaidi katika msururu wa viongozi wakuu katika utawala wa Trump kujiuzulu au kufutwa kazi, tangu Trump alipochukua hatamu za uongozi.
Je, Barua ya kujiuzulu inasemaje?
Kwa njia ya barua kwa Bwana Trump moja kwa moja, ameelezea maoni yake kuhusu "namna ya kuwaheshimu washirika wa Marekani" na matumizi ya "vifaa vyote vya nguvu ya utawala wa Marekani ili vitumike kutoa ulinzi imara".
"Kwa sababu una haki ya kuwa na Waziri wa ulinzi, ambaye maoni yake yanafaa yanafaa kwenda sambamba na maoni yako ya swala hili au lile, nina amini ni sawa tu niachie madaraka niliyo nayo kama Waziri. " aliandika.
Huku akijiepusha kutaja moja kwa moja hatua ya kuyaondoa majeshi ya Marekani nchini Syria, Jenerali Mattis awali alionya kuwa hatua ya kujiondoa haraka kutoka nchi hiyo, kutakuwa"pigo kubwa sana".
Wanajeshi wa Marekani wamekuwa sana maeneo ya Wakurdi, kaskazini mwa Syria
Aidha anaonekana pia kutofautiana na Trump kuhusu maswala kadhaa kama vile Urusi na Nato.
"Maoni yangu ya namna ya kutowaheshimu washirika wetu na pia kusema mambo bayana bila ya kuwaficha wadau wenzetu, na pia mikakati na washindani wetu, yanafaa kulindwa mno na kufahamishwa ipasavyo hasa sawa na ilivyokuwa katika miongo minne iliyopita, kuhusiana na masuala haya," Jenerali Mattis aliandika kwenye barua hiyo.
Aidha, amethibitisha kuwa, ataendelea kuchapa kazi hadi mwisho wa mwezi Februari, ili "kutoa fursa kwa mrithi wake ateuliwe na kupewa kazi".
Comments
Post a Comment