Timu ya Ulimwengu imepangwa Kundi D na Simba SC, CAF Champions League


Ijumaa ya December 28 2018 ndio siku ambayo imecheshwa droo ya Makundi ya michuano ya CAF Champions League msimu wa 2018/2019, Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla tunawakilishwa na Simba SC kutokea Tanzania.

Simba SC leo baada ya droo kuchezwa imejikuta ikipangwa Kundi D na timu za Al Ahly ya Misri, Js Saouro ya Algeria na AS Vita Club ya Congo DRC, makundi yapo manne na timu 2 kila kundi zitapata nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali kama zitafanikiwa kumaliza nafasi ya kwanza na pili.

Kama hufahamu hii ni fursa nyingine kwa mchezaji wa kitanzania Thomas Ulimwengu kurudi Tanzania kucheza katika ardhi ya nyumbani kwao akiitumikia JS Saouro ya Algeria aliyojiunga nayo hivi karibuni na kwakuwa wamepangwa Kundi moja na Simba ni wazi JS Saouro watakuja Tanzania.



Comments