Pusha T baada ya Drake kukosekana kwenye ‘Rap Album Of The Year 2019’


Rapper Pusha T amtolea povu Drake  hii ni baada ya mahojiano aliyoyafanya na Associated Press na kusema kuwa ”Nafikiri kila mmoja anatakiwa kukaa kwenye kipengele chake anachostahili”

Jibu hilo la Pusha T limekuja baada ya Drake kukosekana kwenye kipengele cha Rap Album Of The Year kwenye tuzo za Grammy 2019 na kusisitiza kuwa hafanani na kile anachokifanya Drake huku jibu lake likitafsiriwa kuwa muziki anaofanya Drake sio Hip Hop.

“Sikushangazwa na drake kukosekana kwenye kipengele nafikiri kila mmoja anatakiwa kukaa kwenye kipengele chake anachostahili, sifikirii kwamba mimi na yeye tupo kwenye kipengele kimoja” >>> Pusha T

Pusha T ametajwa kuwania katika kipengele cha Best Rap Album kwenye Grammy 2019 kupitia Album yake ya ‘Daytona

Comments