Jana December 15, 2018 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa, amezindua Chaneli mpya ya Utalii inayoitwa Tanzania Safari Channel, katika studio za TBC, Mikocheni, Jijini DSM.
Chaneli ya Safari imeanzishwa kwa ushirikiano wa TBC na wadau wengine wa utalii wakiwemo Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Uhifadhi Ngorongoro (NCAA) na Bodi ya Utalii Tanzania na itaanza kurusha vipindi vya majaribio kuanzia leo.
Mchakato wa kuanzisha chaneli hii ulihusisha pia mikutano na wadau wa sekta binafsi ambao shughuli zao zinahusiana na masuala ya utalii.
Aidha, Tanzania Safari Channel ambayo lengo lake ni kutangaza vivutio vya utalii nchini itarusha matangazo yake kutokea Mikocheni kwa muda na hatimaye itahamia Dodoma baada ya jengo la TBC Makao Makuu kujengwa.
Comments
Post a Comment