Ben Pol akutana na aliyekuwa mchezaji wa Man United, Memphis Depay

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amekutana na aliyekuwa mchezaji wa Manchester United ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Olympique Lyon, Memphis Depay.

Ben Pol akiwa Dubai amekutana na mchezaji huyo ambaye wiki hii ametoa video ya wimbo wake unaoitwa ‘No Love’.

Siku za hivi karibu Ben Pol ameonekana kuanza kula bata la aina yake ikiwa ni siku chache baada ya taarifa kuzagaa kwenye mitandaoni ya kijamii kwamba anatoka kimapenzi na binti wabilionea wa Kenya, Tabitha Karanja aitwae, Anerlisa Muigai.


Binti huyo akiwa na Mama yakeambaye anamiliki kiwanda cha kutengeneza bia kiitwacho, Keroche Breweries.


Muimbaji huyo ambaye kwasasa anafanya vizuri na wimbo, Sio Mbaya ameonekana kuwa karibu zaidi ya binti huyo ambaye ni bosi wa kampuni ya kutengeneza maji ya chupa iitwayo, NERO company ambayo inazalisha maji ya Executive.

Hata hivyo kwa sasa staa huyo amekuwa akifanya matamasha mbali mbali barani Ulaya.

Comments