Alikiba akishirikiana na baba yake Samatta, wakabidhi vifaa hivi , kuhitimisha kampeni ya NIFUATE

Kampeni ya iliyoanzishwa na msanii wa muziki wa Bongo fleva pia akiwa mshambuliaji wa klabu ya Coastal Union ya Tanga, Alikiba akishirikiana na mchezaji wa mpira wa miguu kutoka katika klabu ya Genk ya Ubelgiji na timu ya taifa ya Tanzania Mbwa Ally Samatta imehitimishwa leo maeneo ya Mbagala jijini Dar Es Salaam.
Image result for alikiba na samatta
Msaada huo kwa shule za msingi ambao uilipangwa kutolewa na mastaa hawa wawili baada ya mchezo wao uliofanyika takribani miezi mitatu iliyopita katika uwanja wa taifa na kuahidi kwamba viingilio vitakavyopatikana basi watasaidia shule mbalimbali nchini Tanzania lakini kwanza waanze na shule walizosomea.


kupitia ukurasa wa Instagram Alikiba ameandika haya:– “Tumefanikiwa kukabidhi zawadi ya meza , viti, na vitabu katika shule ya Mchikichini iliyoko Mbagala rangi Tatu Nikishirikiana Na muwakilishi wa @samagoal77 Mzee samatta (BABA)Tunamuomba MUNGU atuongoze Tuweze Kuendeleza Msaada Huu mashuleni

Comments