Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kulitoa taifa la Marekani katika Shirika la Biashara Duniani WTO iwapo shirika hilo litashindwa kubadilisha mfumo wa utendaji wake kazi kwa taifa hilo kubwa Duniani.
Akihojiwa na Jarida la Bloomberg Rais Trump amesema iwapo halitajirekebisha atajiondoa katika WTO.
Rais Trump amekuwa akishinikiza sera zinazoitetea nchi yake akisema kuwa Marekani inashuighulikiwa isivyo sawa na shirika hilo.
Shirika hilo la Biashara duniani lilianzishwa kwa ajili ya kusimamia sheria za biashara duniani na kutatua tofauti kati ya nchi.Onyo lake hilo alilolitoa la nchi yake kuweza kujitoa katika Umoja huo umeonesha mvutano uliokuwepo kati ya sera za kibiashara za Rais huyo na mfumo wa biashara huru ambao shirika hilo unasimamia.
Kama hiyo haitoshi hivi karibuni Marekani ilipinga uchaguzi wa majaji wapya wa mfumo wa WTO wa kukabiliana na mashauri jambo ambalo linaweza kudhorotesha uwezo wa kutoa hukumu.
Mwakilishi wa Markani katika masuala ya biashara Robert Lighthizer naye amekuwa akiinyoshea kidole WTO kwa kuingilia mamlaka ya Marekani,Mwaka jana Rais Trump alinukuliwa na Shirika la Habari la FOX kuwa WTO inanufaisha wote isipokuwa Marekani.
Chanzo BBC

Comments
Post a Comment