Samatta apiga ‘hat-trick’ Europa League, mwenyewe aeleza matarajio yake

Mshambuliaji hatari zaidi ndani ya klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji raia wa Tanzania, Mbwana Samatta hapo jana aliiandika historia mpya katika soka lake baada kutupia ‘hat-trick’ yake ya kwanza tangu kujiunga na miamba hiyo akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wake dhidi ya Brøndby IF kutoka Denmark michuano ya  Europa League.

Katika mchezo wa uliyopigwa hapo jana dimba la Luminus The Arena KRC Genk, Samatta aliifungia mabao klabu yake dakika 37, 55, na 70 huku mabao mawili yakifungwa na Mbelgiji Leandro Trossard dakika ya 45 na 90 wakati mabao yale ya Brøndby IF yakifungwa na Hermannsson dakika ya 47 na Wilczek dakika 51 na mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa jumla ya magoli 5-2.

https://www.instagram.com/p/Bm1wzMxlqv_/?taken-by=samagoal77
Video: Samatta kama kawaida awanyoosha Lech Poznan michuano ya Europa League
Katika hali ya kueleza matumaini yake Samatta ameandika kuwa mashabiki watarajie hat-trick nyingine zinafuata baada ya hizo za jana.

"Nna furaha kufunga hat-trick yangu ya kwanza nikiwa na genk usiku wa leo,naimani nyingine nyingi zinafuata. HAINA KUFELI
…..proud with the team & happy with our fans, also happy with my 1st hat-trick with genk, on to the next one. Forza racing"



Comments