CCM wawachinjia baharini wasanii wa Bongo Fleva, wadai hawatawatumia tena kwenye kampeni zao

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema kuwa kwenye kampeni zake za chaguzi zijazo hawatatumia tena wasanii wa muziki wa Bongo Fleva badala yake watatumia bendi ya TOT kwani nyimbo zao zina ujumbe mahususi kwa Watanzania.
Image result for Dkt. Bashiru Ally
Dkt. Bashiru Ally

Akiongea na Waandishi wa Habari Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally akifungua kikao cha Baraza kuu la UVCCM jijini Dodoma leo Agosti 30, 2018 amesema CCM haitakuwa tena na bajeti ya wasanii kwenye kampeni zijazo.

“Hatutakuwa na bajeti ya wasanii tena, hakuna. Tutabaki na TOT tutaendesha chombo chetu kile kama alama na vijana JAZZ basi, tukienda Arusha tutawakuta wasanii kule. Wataimba mashairi watacheza ngoma. Nilipofika hapa makao makuu niliwakuta watu wanapiga zeze hapa inapendeza sana kuliko haya ya kuruka ruka na kucheza cheza sio mabaya, lakini kikubwa sio haya ya kuruka ruka ila ujumbe uliopo mule, hisia zinazotokana na wimbo ule.“amesema Dkt. Bashiru.

Kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015, CCM iliwatumia wasanii wa Bongo Fleva kibao ikiwemo Diamond Platnumz, Alikiba, Fid Q na wengineo.

Comments