Msanii wa muziki wa hip hip, Young Dee amefunguka kuzungumzia post ambayo aliiweka mitandaoni inayohusiana na kutaka kumsaini rapa Young Killer Msodoki ambaye kwa sasa anafanya kazi chini ya label ya Wanene Entertainment.
Young Dee
Dee ambaye kwasasa anafanya kazi na label ya King Cash, kupitia instagram aliandika “Hahaha siku ya kwanza ofisini wakati nataka kumsign mdogo wangu #youngkillermsodokii 😀😀 ni kweli anachana sana kijana ana kipaji!,”
Baada ya kauli hiyo hotmixmziray ilimtafuta na kuzungumza naye kuhusiana na kauli ambapo alidai hakuna kitu ambacho kinashindikana kwenye hii dunia.
“Young Killer ni rapa mzuri sana, namkubali sana lakini ishu za kumsaini ni mapema sana pale niliandika kama masihara lakini mimi nadhani ni jambo ambalo linawezekana kama nikiamua kwa sasabu ana kila kitu,” alisema Young Dee.
Young Dee na Young Killer wote kwa pamoja watashiriki katika tamasha kubwa la muziki la Sports Muziki Festival linalotarajiwa kufanyika Mwanza, Geita na Kahama katika ya mwezi huu.

Comments
Post a Comment