Label ya WCB ipo katika mchakato wa kuongeza msanii mwingine wa kike.
Hatua hiyo inakuja baada ya kipindi kirefu Queen Darleen kuwa ndiye msanii pekee wa kike katika label hiyo.
Miongoni mwa mameneja wa WCB, Babu Tale katika mkutano na waandishi wa habari alieleza kuwa hilo limekuwa likiuliziwa kwa siku nyingi kwanini WCB hakuna msanii mwingine wa kike, hivyo sasa wameona ni wakati wa kushughulikia hilo.
“Nimetoka kusemwa juzi, tukaambiwa tuongeze msichana mpya nikawaambia hapana, muda ukifika tutaongeza,” amesema.
“So tutaongeza haya ni maoni yenu ambayo mmekuwa mkitusapoti, tutakuja kuongeza msanii wa kike ambaye tunajua mtamfurahi wote,”
Kwa kipindi alichokuwa WCB, Queen Darleen ameweza kuachia ngoma kama Kijuso, Ntakufilisi, Touch na kushiriki kwenye wimbo ‘Zilipendwa’ ambao uliwakutanisha wasanii wote wa label hiyo.
Comments
Post a Comment