Si WCB pekee; RC Makonda asema fursa ni kwa wote

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema yeye ni mlezi wa wasanii wote na si wale wa WCB pekee.

Akizungumza katika Futara aliyoandaa jana Mlimani City alisema kuwa amekuwa mlezi wa WCB kwa vile walimuomba kufanya hivyo ila haimaanishi hayupo na wasanii wengine.

“Mimi ni mlezi wa wasanii wote lakini wasanii kuomba tunataka asilimia mia moja utusimamie uamuzi ni wao, Mkuu wa Mkoa ni mlezi wa kila msanii,” amesema.

“Kwa hiyo wao waliomba, ebu tusaidie kutuangalia na sisi tukiwa chini yako tunatumaini tutafanya vizuri na mimi nikasema karibuni,” amesisitiza.

Kwa kipindi sasa RC Makonda amekuwa mlezi wa WCB na wamekuwa pamoja katika kampeni mbali mbali kama ile uchangiaji madawati ambapo Diamond Platnumz alichangia madawati 600.

Comments