Rais Magufuli :Kuna Vilaza wanaajiriwa nawaona


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameinyooshea kidole wizara ya kazi na ajira kuwa kuna watu wameajiriwa lakini wanafanya kazi chini ya kiwango jambo ambalo hapendezwi nalo.


Rais ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akipokea gawio la Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania (TTCL) , ambapo amesema kuwa suala hilo ameliona na amewaachia wabunge walitazame kwa mapana.


“Wizara ya Kazi kuna matatizo matatizo huko, nimeshayaona, nimeanza kuyafuatilia, kuna wengine vilaza kabisa lakini wanaletwa huko kuja kufanya kazi, hili nitalishughulikia, nalichomekea tu ili wabunge walitazame”, amesema Rais Magufuli.


Wizara hiyo ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) inaongozwa na Waziri Jenista Mhagama, pamoja na Naibu wake Anthony Mavunde.

Comments