Nuh Mziwanda ‘achomoa’ kuhusu Amber Lulu na Shilole

Msanii wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda amefunguka kuhusu mahusiano yake na Amber Lulu na iwapo kwa sasa ana ukaribu na aliyekuwa mpenzi wake, Shilole.
Muimbaji huyo akipiga stori na Wasafi TV amesema kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na Amber Lulu kama inavyodhaniwa.

Kauli ya msanii huyo inakuja baada ya hivi karibuni kuvuja kwa video mtandaoni ikimuonesha akiwa na Amber Lulu katika mahaba mazito.

“Sijawahi kuwa na mahusiano na Amber Lulu, mabwana zake wengi pia ni watu ambao mimi nawafahamu. Hata siku kinafanyika kile kitu bwana yake mmoja alikuwepo,” amesema Nuh.

Alipoulizwa iwapo amewahi kwenda kula kwenye mgahawa ‘Shishi Ford’ wa aliyekuwa mpenzi wake, Shilole, alisema ni kitu ambacho hawazi kukifanya.

“Siwezi hata kukanyaga mguu wangu pale, siwezi na siwezi kwenda pale kula, hata mama yangu anajua kupika,” amesisitiza.

Utakumbuka baada Nuh Mziwanda kuachana na Shilole alifunga ndoa na binti aitwae Nawal hata hivyo walikuja kuachana. Baadae kabisa Shilole naye alikuja kuolewa na Uchebe.

Comments