Baada ya producer Mkongwe Bongo, P Funk Majani kueleza kuwa ameka tamaa na sanaa ya Bongo hadi kufikiri kwenda kufanya kazi zake nje, rapper Nikki Mbishi ameeleza anapofeli producer huyo.
Awali P Funk akipiga stori na Clouds TV alieleza kuwa amekuwa hasikiki kwa sasa kutokana na changamoto zilizopo kwenye game ingawa mchango wake ni mkubwa katika muziki huo.
“Inanikatisha tamaa na hadi sasa hivi nataka niweke vitu sawa labda nikajaribu Amerika kwa sababu muda unaenda, nazeeka,” alisema P Funk.
Sasa Nikki Mbishi ameeleza kuwa P Funk amefikia hatua hiyo kutokana na kuanza kufuata trend, majina na fedha na sio vipaja. Kupitia Instagram ameandika;
Majani tatizo siku hizi huamini vipaji vikali tena unaamini majina tu na hela ndio maana yanatokea hayo,we still have that opportunity to make it since giving up ain’t an option.
Unaacha kutupa midundo mikali wenye contents zetu una-deal na trends na kiki za akina Harmorapa, I find no use for you to complain.Unadhani hatupendi kufanya kazi na wewe?.
Hata hivyo Nikki Mbishi amekuwa si rapper wa kufanya kazi sana na ma-producer wakongwe, mara nyingi amesikika kwenye midundo ya ma-producer kama Duke Tachez, Texa, Mujwahuki, Palla Midundo, Bunduki Midundo, Teknohama na wengineo.
Comments
Post a Comment