Kuna baadhi ya makundi hayapewi nafasi kwenye media-Roma

Msanii wa muziki Bongo, Roma amesema sababu ya baadhi ya wasanii wakongwe kutopenda kuitwa hivyo ni kutokana na kutopewa nafasi katika vyombo vya habari na kuonekana wakati wao umepita.
Related image

Roma katika mahojiano na FNL ya EATV ameeleza kutokana na hilo wasanii hao wana haki ya kukataa kuitwa wakongwe.

“Unafikiri ishu ni ukongwe, wala si hivyo, ishu ni kuna baadhi ya makundi hayapewi nafasi kwenye media house, mchongo ndio upo hapo, hizo nyingine zote mchongoma tu,” amesema.

“Snoop Dog ni mzee anafanya mchongo na Wiz Khalifa, kwanini Mox asifanye mchongo na Country Boy halafu ukawa kweli mchongo lakini sisi tunakuja kuitafsiri mkongwe hana nafasi kwenye generation ya sasa hivi which is total wrong,” ameongeza.

Ameendelea kwa kusema ikiwa msanii ataitwa mkongwe lakini anapata kile ambacho anastahili wala hakuna ambaye angelaumu ila kwa namna inavyotafsiriwa na watu wa vyombo vya habari sivyo.

Comments