Zinedine Zidane atangaza kuondoka Real Madrid

Meneja wa klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane ametangaza kuondoka Bernabeu ikiwa ni siku chache tu tangu kuipatia ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya Jumamosi iliyopita na kuwa kocha wa kwanza kutwaa taji hilo mara tatu mfululizo.

Zidane mwenye umri wa miaka 45, ameiyongoza Real kutwaa taji lake la nne la klabu bingwa barani Ulaya ndani ya miaka mitano na huku ikichukua mara tatu mfululizo chini ya uongozi wake baada ya kuwafungwa Liverpool huko Kiev siku ya Jumamosi iliyopita licha ya Los Blancos hao kuishia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa LaLiga.

Mfaransa huyo  aliyerithi mikoba ya Rafael Benitez  Mwezi Januari mwaka 2016 amekuwa katika shinikizo kubwa la kutwaa taji la La Liga ndani ya miaka yake miwili na nusu aliyokuwa akiiongoza Madrid.

Mwezi Januari mwaka huu, Zidane alithibitisha kusaini kandarasi ya miaka miwili ambayo ingemfanya kusalia hapo mpaka mwaka 2020 jambo ambalo amesema kuwa halina maana yoyote kwake.

Comments