TFF YAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWAPA SIMBA FC KOMBE



Leo May 15 2018 Rais wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia kupitia vyombo vya habari ametangaza rasmi kuwa shirikisho la soka Tanzania TFF limeandika barua kwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe kumuomba Rais Magufuli ahudhurie uwanja wa Taifa katika utoaji wa Kombe kwa Simba.

Jumamosi ya May 19 Simba SC watacheza mchezo wao wa Ligi Kuu  dhidi ya Kagera Sugar wakiwa tayari wameshatangazwa Mabingwa hivyo TFF imemuomba Rais Magufuli kuhudhuria kama mgeni rasmi na kuikabidhi Simba Ubingwa wa VPL msimu wa 2017/2018.

Hata hivyo TFF pia imemuomba Rais Magufuli kabla ya mchezo huo akubali kupokea Kombe la Ubingwa wa CECAFA U-17 kutoka kwa timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys kwa vijana hao ambao walishinda nchini Burundi, kama Rais Magufuli atakubali kuwa mgeni rasmi na kuhudhuria mchezo wa Simba ndio itakuwa mara yake ya kwanza kwenda uwanjani kuangalia mechi toka aapishwe kuwa Rais wa Tanzania November 5 2015 ikiwa ni miaka miwili na siku 186 imepita toka awe Rais.

Comments