Mbunge wa jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma kupitia tiketi ya Chadema, Mh. Kasuku Samson Bilago amefariki dunia.
Mh. Bilago amefariki mchana wa leo May 26, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, ambapo ameeleza kuwa taarifa zaidi juu ya msiba huo zitatolewa muda si mrefu.
Marehemu alizaliwa February 02, 1964 alikuwa mwanachama Chadema na alichaguliwa kuwa mbunge wa Buyungu kuanzia mwaka 2015 hadi mauti yalipomkuta, pia alikuwa ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi.
Comments
Post a Comment