Riyama Ally afunguka maisha nje ya filamu, ‘Uzuri tunapiga miguu yote’

Msanii wa filamu Bongo, Riyama Ally amesema msanii anapoamua kufanya biashara haimaanishi kuwa sanaa anayofanya haimlipi.

Kauli ya msanii huyo imekuja mara baada kujiingiza katika biashara ya nguo (t-shirt).

Riyama amesea kuwa msanii hapaswi kutegemea sanaa pekee kama njia ya kujiingizia kipato na ndio sababu ya yeye kufanya hivyo.

“Hapana sio kweli, mtu unatakiwa kufanya vitu mbali mbali ili kuweza kujiongezea kipato lakini movie na tamthilia zinalipa na uzuri tunapiga miguu yote, basi mambo mazuri hiyo nimejiongeza tu,” Riyama Ally ameiambia hotmixmziray.

Ukiachilia mbali filamu na biasha ya nguo, pia Riyama Ally ni balozi wa kampuni kubwa mbali mbali za Bongo na nje.

Comments