Kuna kipindi Mpiga picha wa Diamond, Lukamba alioneka katika picha moja na mwanamitindo Hamisa Mobetto wakati huo Diamond na Zari bado walikuwa na mahusiano kitu ambacho kilileta maneno.
Sasa Lukamba amefunguka kile kilichotokea kwa kueleza kuwa alikutana na Hamisa kwa ajili ya ku-shoot kipindi cha Wasafi TV na hakukuwa na zaidi ya hapo kama ilivyokuwa ikienezwa.
“Japokuwa watu walinitukana mtandaoni lakini mimi nafanya kazi, boss wangu ana TV kwa hiyo akiniambia Lukamba kam-shoot na si sikum-shoot Hamisa pekee yake na nilivyomaliza picha ni kitu cha kawaida lakini watu walivyoipokea ilikuwa tofauti,” Lukamba ameiambia hotmixmziray
Kilichofanya ishu hiyo kuwa kubwa ni kutokana Hamisa Mobetto na Zari The Boss Lady hawaelewani baada ya Hamisa kuzaa na Diamond huku akifahamu fika muimbaji huyo bado alikuwa na mahusiano na Zari.
Comments
Post a Comment