Manara aahidi mazito klabu bingwa Afrika ‘Mwakani Rais atatualika Ikulu kwa kazi tutakayoifanya’


Mara baada ya Rais Magufuli kwenye hotuba yake hapo juzi kuwasifia Kagera Sugar kwakuonyesha mchezo mzuri uliyozaa ushindi dhidi ya Simba huku akiwaambia mabingwa hao kwakiwango walichoonesha hawataweza kutwaa ubingwa wa Afrika, afisa habari wa timu hiyo Haji Manara amekiri kutochukua taji hilo kwa namna kiwango chao kilivyo na kuahidi kufanya vema mwakani kwenye michuano hiyo mikubwa ya Afrika hali itakayopelekea kualikwa Ikulu.




Manara ameyasema hayo jana usiku kupitia kipindi cha Mshikemshike Viwanjani kinachoruka kupitia Azam Tv.

Hatuwezi kuchukua ubingwa wa Afrika kwa namna tulivyocheza juzi nikweli, sio huko tu Ndondo Cup tunaweza tukaingia na tukapigwa, juzi hatukucheza vizuri kabisa.

Kwa hiyo sisi tumuahidi Rais Magufuli tumeisikia kauli yake na tutaifanyia kazi, tutaboresha pale panapo stahili lakini kuhusu ubingwa wa Afrika alilotoa ni agizo tunalifanyia kazi namuahidi mwakani Mwenyezimungu akitupa uhai na majaaliwa siyo kuja tu yeye uwanja wa taifa, atatualika Ikulu kwa kazi tutakayo ifanya ninaahidi shikeni kauli yangu mwakani mtaniekea.

Msemaji huyo mwenye mbwembe, vituko na maneno mengi hali inayompelekea kupendwa zaidi na mashabiki wa Simba ameonekana juzi kuchanganyikiwa uwanjani mara baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi kukosa mkwaju wa penati dakika ya lala kwa buriani ambayo endapo ingeingia kwenye lango la kipa Juma Kaseja mechi hiyo ingekuwa imeamuliwa kwa sare ya bao 1 – 1.


Comments