Madee akinzana na Diamond kuhusu mwanae kufanya muziki

Msanii wa muziki Bongo kutoka Tip Top Connection, Madee amesema iwapo wanae wa kike, Aimal Hamad  atachagua kuwa msanii kama yeye hatokataa kwa sababu na yeye pia amefuata nyayo za baba yake.

Mtazamo wa Madee unatofautinaa na ule wa Diamond Platnumz pale alipoulizwa kuhusu mwanae Tiffah kuja kufanya muziki. Katika mahojiano na KTN, May 2017 alisema anaogopa iwapo Tiffah ataingia katika muziki ataweza atembea kimapenzi na wanaume wengi.


Sasa Madee katika mahojiano na Bongo5 hivi karibuni alisema licha ya mara nyingi kuwa na wanae hata studio hajui iwapo atapenda muziki lakini yeye kama mzazi hawezi kumuwekea mipaka.

“Tunashauriwa tuwaangalie watoto wafanye kile ambacho wanapenda kwa sababu anaweza kuwa anapenda mpira mimi nikamzuia nikamwambia afanye kitu kingine na asifanikiwe, nitakuwa nimepata lawama,” amesema.

“So akielekea huko mimi sina tatizo kwa sababu hata mimi mwenyewe nimemfuata baba yangu alikuwa ni mwanamuziki wa Western Tabora Jahazi Band wala hakutegemea nitakuwa mwanamuziki, so sitaona maajabu sana kwa sababu Waswahili wanasema maji hufuata mkondo,” Madee ameiambia Bongo5.

Mtoto wa Madee, Aimal Hamad ni miongoni mwa watoto wa wasanii ambapo pia wanapatikana katika mtandao wa Instagram.

Comments