Maamuzi ya Mahakama yapelekea msanii ‘Kiss Daniel’ kutoka Nigeria kubadilisha jina lake

Kama wewe ni Mwandishi wa Habari za Burudani au ni mtangazaji wa Radio/Tv basi hautaruhusiwa tena kuandika au kutamka jina la Kiss Daniel kwenye kazi zako kama ilivyokuwa awali na kufanya hivyo utakuwa umetenda kosa.
Image result for kiss daniel images

Kizz Daniel ambaye zamani alikuwa anaitwa Kiss Daniel

Kiss Daniel kuanzia jana Mei 22, 2018 alibadilisha jina lake na kujiita KIZZ DANIEL hii ni baada ya kumaliza mgogoro wake mahakamani na lebo iliyokuwa ikimsimamia mwanzoni ya G-Worldwide Entertainment .

Mwaka jana Kizz Daniel alikiuka masharti ya mkataba wake na G-World Ent. kwa kutangaza kufungua lebo yake ya Flyboy Inc, jambo ambalo lilipelekea uongozi wa G-World Entertainment kumfungulia mashtaka Kizz Daniel.

Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu Mahakama mjini Lagos ilimpiga marufuku msanii huyo ku-perfom nyimbo zake zote alizotoa kipindi yupo chini ya lebo hiyo au kutumia jina lake kibiashara mpaka kesi itakapomalizika.

Kwa sasa Kizz Daniel tayari ameshabadilisha jina lake lililozoeleka la Kiss Daniel kwenye platform zote za muziki na kurasa zake za mitandao ya kijamii kama mahakama ilivyoamuru.


KIZZ DANIEL

@iamkissdaniel
 “Walk away from anything that gives you bad vibes. You don’t have to make sense of it or make clear. It’s ur life, do what makes you happy ” 😊
4:13 PM - May 23, 2018
833
369 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy






Comments