kila mtu anapenda kusaidiwa lakini kuna misaada mingine mpaka mtu unajuta – Shamsa Ford

Nani amemuudhi Shamsa Ford? Msanii huyo wa filamu Bongo ameonyesha kukerwa na tabia za baadhi ya watu ambao wanatoa misaada na baadae kuwafanya wenzao kama matangazo.

Shamsa ameonekana kutupia jiwe hilo gizani ambalo tayari limempata ambaye alimkusudia. Shamsa amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagarm.

kila mtu anapenda kusaidiwa lakini kuna misaada mingine mpaka mtu unajuta kwann umesaidiwa. utafanywa tangazo kila sehemu,utasemwa na kusimangwa kila sehemu,utafanywa mtumwa,hata kama akikuudhi itabidi tu umchekee, Huyo mtoa msaada atajiona Mungu MTU kwamba bila YEYE maisha hayaendi, hapo bado hajakubania sehemu utasema yeye ndo mtoa RIZIKI. Misaada ya aina hiyo ni bora ikupite ufe na shida zako tu maana itafika sehemu utamsujudu yeye na kumsahau Mwenyezi Mungu ..

Comments