Jibu la Hamisa kuhusu tuhuma za ‘kudundwa’ na mama Diamond

Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka kuhusu taarifa zilizodai kuwa amepigwa na mama mzazi wa Diamond Platnumz, Sanura Kassim ‘Sandra’.

Hapo jana katika uzinduzi wa kipindi cha Nyumba ya Imani cha Wasafi TV, Hamisa alipata time ya kuzungumza na waandishi wa habari na kusema jambo hilo ni binafsi zaidi ila kugombana kwa binadamu ni kitu cha kawaida.

“Hilo siwezi kuliongelea, yeah!. is too person, is too private, is too family. Hata vikombe kwenye kabati vinagong’ana, so sisi binadamu vinaweza kutokea,” amesema.

Alipoulizwa iwapo kwa sasa yeye na mama Diamond wana maelewano mazuri, alijibu; ‘Sina kinyongo na mtu, sina bifu na mtu, mimi am just fine, may be yeye mwenyewe sio upande wangu wa kuweza kuelezea,’.

Taarifa za Hamisa kupigwa na mama Diamond zilianza kusambaa Jumatatu ya wiki iliyopita, May 14, 2018 ambapo usiku ya jana yake Hamisa na Diamond walihudhuria katika uzinduzi wa filamu ya Aunt Ezekiel ‘Mama’ na baada ya hapo anadaiwa waliongozana hadi Madale kwa kina Diamond ambapo ndipo kisa hicho kinadaiwa kutokea.



Comments