Hatma ya Mrisho Ngassa kurejea Yanga yabaki mikononi mwa benchi la ufundi

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika umesema kuwa huwenda ikamrejesha mchezaji wake wazamani, Mrisho Khalfan Ngassa kwenye kipindi hiki cha usajili baada ya benchi la ufundi kukaa na kuangalia hilo.

Usajili wetu kuanzia mwaka juzi tumekuwa tukifanya siri mpaka pale dili linapotimia ndiyo tunaweka wazi lakini tumeshafanya mazungumzo kwa wachezaji wa ndani na nje ya nchi.

Mrisho Ngassa kurejea Yanga nimesikia kupitia kwenye vyombo vya habari lakini niwaambie wapenda soka na wapenzi wa Yanga, Ngassa ni mchezaji mzuri na kila mtu ameona uwezo wake mwaka huu na isitoshe anamapenzi sana na Klabu kwahiyo lolote linaweza kutokea.

Lolote linaweza kutokea kurudi ama kutorudi Yanga, hakuna mtu ambaye hatambui uwezo wa Ngassa kwa mwaka huu ulivyokuwa mkubwa sana lakini pia ana mapenzi makubwa na klabu ya Yanga kwahiyo viongozi na benchi la ufundi litakaa chini na kuangalia kama wanamuhitaji.



Ngassa ambaye aliwahi kupita kwenye klabu za Azam FC na Simba SC amepata kuitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa katika ligi kuu soka Tanzania Bara, amepata pia kuichezezea Mbeya City FC kisha kutimkia Ndanda FC ya Mtwara.

Comments