TETESI: Wanandoa Prince Harry na Meghan kufanyia ‘Honey Moon’ Afrika, nchi mbili zatajwa

Ikiwa ni siku moja imepita tangu harusi ya kihistoria ya kifalme ifanyike nchini Uingereza, kati ya Prince Harry na Meghan Markle sasa maswali mengi yanakuja ni wapi wanandoa hao watakwenda kwa ajili ya fungate (Honey Moon).

Prince Harry na Meghan Markle

Kwa mujibu wa mtandao wa Travel + Leisure umeeleza kuwa wawili hao huenda wakaja Afrika kwa ajili ya fungate na nchi zilizotajwa ni Namibia na Botswana.

Hata hivyo, vyanzo vingi vya habari vinaitaja nchi ya Namibia kuwa ndiyo itakuwa sehemu ya kwanza kwa wawili hao kupumzika kwa ajili ya fungate.

Mwaka 2017 kwenye birthday ya Meghan, wawili hao walienda nchini Botswana kwa ajili ya kusherehekea siku hiyo ya mfanano wa kuzaliwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa jarida la Vogue, bajeti ya Honey Moon kwa wawili hao ni Dola $221,175 sawa na tsh milioni 505.

Wawili hao kabla ya kuanza fungate wanatarajiwa kwenda nchini Mexico kumuona baba mzazi wa Meghan, Thomas Markle (75) ambaye hakuhudhuria kwenye harusi kutokana na maradhi ya moyo yanayomsumbua kwa muda mrefu.


Comments