Diamond na Vanessa Mdee watajwa kuwania tuzo za African Pride Awards 2018

Wasanii wa Bongo Flava Diamond na Vanessa Mdee wametajwa kuwania tuzo za African Pride Awards 2018 ambazo zitafanyika June 3, 2018 London Uingereza.

Diamond Platnumz ametajwa kuwania kipengele cha African Male Artist Of The Year ambapo atachuana na wasanii kama Ido West, Davido, Wizkid, Mayorkun, Slimcase, Shatta Wale, Cassper Nyovest, Kiss Daniel, Eddy Kenzo, Nasty C, Dice Ailes na Burna Boy.

Kwa upande wa Vanessa Mdee atawania kipengele cha African Female Artist Of The Year ambapo atapambana na wasanii wenzake kama Tiwa Savage, Niniola, Seyi Shay, DJ Cuppy, Becca, Ebony, Yemi Alade na Teni.

Pia Official DJ wa Diamond Platnumz, Romy Jons ametajwa kuwania kipengele cha Outstanding International Disc Jockey of the Year.


Comments