Diamond akunwa na Mrisho Mpoto alivyobadilika kupitia wimbo ‘Nimwage Radhi’

Hakuna aliyetegemea kama msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto angeweza kutoka na kibao cha wimbo ‘Nimwage Radhi’ akiwa tofauti na kukubalika kila kona na mashabiki wa muziki wake.

Muimbaji huyo alizoeleka na nyimbo kama Sizonje, Njoo Uichukue, Mjomja pamoja nyingine nyingi lakini safari hii akiwa na Harmonize kutoka WCB amekuja wimbo tofauti kabisa ambao unafanya vizuri kupitia mtandao wa YouTube.

Rais wa WCB, Diamond ameonekana kufurahishwa na kitendo hicho na kuamua kummwagia sifa muimbaji huyo.

“Kwa kweli Mrisho Mpoto nilikuwa nakuwaza sana, Kwa ufanisi wa serikali hii, ungewezaje kutupa vile vibao vyako vya #MJOMBA #WAITE Na Kadharika…. ila nimeamini kweli Mungu kakutunuku Kipaji na Ubunifu wa Sanaa, Sikutegemea kama UtaniSurprise namna hii… #NimwageRadhi Kali sana🙏🙏 ….Mdogo angu Mmakonde @harmonize_tz naona Mwaka Huu unahasira nao sana….Kama Naiona hiyo #WasafiFestival Huu Mwaka Sjui hata tuanzie Mkoa gani???,” aliandika Diamond Instagram.

Naye Mkuu wa mkoani wa Dar es salaam, Paul Makonda alimmwagiza sifa muimbaji huyo kutokana na kibao.

Kwa sasa video ya wimbo huo inashika nafasi ya pili kupitia mtandao wa YouTube.

Comments