Mahakama moja ya India imemhukumu nyota muigizaji wa sinema za Bollywood Salman Khan, hukumu ya miaka mitano jela kwa kuua aina mojawepo ya swala ambao ni adimu kupatikana duniani mwaka 1988.
Mahakama hiyo iliyoko Jodhpur imemtoza faini ya rupia 10,000 ($154; £109) kwa kosa hilo.
Amepelekwa korokoroni na anatarajiwa kusalia huko kwa muda.
Khan aliwaua swala wawili kwa jina blackbucks, ambao hulindwa na kuhifadhiwa, Magharibi mwa jimbo la Rajasthan alipokuwa akiigiza filamu.
Waigizaji wengine wanne walioshiriki naye uigizaji kwenye filamu hiyo, waliokuwa wamehukumiwa kwa kosa hilo na mahakama ya awali, walisamehewa.
Khan, 52 , anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama ya juu.
Wanahabari wamesema atasalia korokoroni kwa siku kadha.
Nini chanzo cha kesi ya Khan?
Hii ni kesi ya nne iliyowasilishwa dhidi ya mwigizaji huyo inayohusiana na uwindaji haramu wa wanyama wakati walipokuwa wakiigiza filamu ya Hum Saath Hain mwaka 1988.
Amesamehewa makosa matatu.
Mwaka 2006, mahakama ilimuhukumu mwigizaji huyo kwa makosa mawili ya uwindaji haramu na kumuhukumu miaka mitano jela. Mahakama ya juu ya Rajasthan ilitupilia mbali uamuzi huo mwaka 2007 na mwaka 2016 ikampa msamaha.
Serikali imekata rufaa dhidi ya uamuzi huo uliotolewa na mahakama kuu.
Kesi halisi ya uwindaji dhidi yake iliwasilishwa na jamii ya Bishnoi ambao wanawaheshimu na kuwaabudu swala hao aina ya blackbuck.
Je, ameshtakiwa kwa kosa jingine?
Mwezi Desemba mwaka 2015, kesi dhidi ya Khan ya kumgonga mtu fukara kwa gari na kutoroka ilifutiliwa mbali.
Watu wengine wanne walijeruhiwa.
Gari lake linadaiwa kuwagonga watu hao walipokuwa wamelala kando ya barabara Magharibi mwa mji wa Mumbai.
Mahakama ya chini ilikuwa imemuhukumu mwezi Mei mwaka 2015.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Khan alikuwa amedai kwamba dereva wake ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo, lakini jaji wa mahakama hiyo alisema mwigizaji huyo ndiye aliyekuwa akiliendesha gari hilo na alikuwa mlevi.
Miezi saba iliyopita, mahakama ya juu ilimsamehe. Ilisema ushahidi ulio bayana unajumuisha ushuhuda kutoka kwa polisi ambaye baadaye alifariki - hauaminiki.
Mwezi wa Januari mwaka 2017, Khan alisamehewa kesi nyengine iliyomhukumu kwa kutumia silaha zilizoharamishwa kuwaua blackbucks.
Salman Khan ni nani hasa?
Ni mwigizaji nyota wa sinema za Bollywood, mwigizaji ambaye ameigiza katika zaidi ya filamu 100 na mwenye ufuasi mkubwa katika jamii yote ya Wahindi.
Mashabiki wake wanawajumuisha watu wenye maisha ya wastani wanaozungumza lugha ya Kiingereza na hata maskini ambao wanaishi kwenye vitogoji duni ambao ni vigumu kupata angalau rupia 350 ($5.20; £3.40) za kununua tiketi .
Muigizaji huyo anafahamika kuigiza majukumu ya mapenzi na hata mwigizaji wa filamu za vita.
Khan ameshinda tuzo kubwa na za hadhi ya juu kwenye tuzo za filamu za India.
Kifungua mimba wake Salim Khan anafahamika kama mwandishi wa filamu na ana wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii - katika ukurasa wake mtandao wake wa Facebook ana wafuasi milioni 36 na Twitter ana wafuasi milioni 32.5.
Comments
Post a Comment