Moja ya wasanii ambao wamekuwa wasiri kwenye mahusiano yake ni Belle 9, hili halina ubishi kwani hata kwenye ishu yake ya kufunga ndoa mwaka jana hakuna chombo cha habari chochote kilipata exclusive zaidi ya yeye mwenyewe kuweka picha za tukio hilo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Ukweli ni kwamba licha ya kuwa msiri Belle 9 ameweka wazi kuwa katika mahusiano yake alishawahi kufumaniwa japo ni sio mara nyingi.
“Nimeshawahi kufumaniwa ila ni mara chache sana, wanawake wengi huwatamani wasanii kimapenzi kutokana na ushwawishi wa wasanii, Mwanamke wangu nataka ajitambue,“ amesema Belle 9 kwenye kipindi cha Tresha’z Dairy cha Radio Kings FM.
Mwaka jana mwezi Desemba Belle 9 alifunga ndoa ya siri mkoani Morogoro na mchumba wake ambaye amedumu naye kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment