Wizkid kukinukisha BET Awards 2017

Black Entertainment Television (BET) wametangaza majina ya wasanii watako tumbuiza usiku wa June 25 Jumapili katika utoaji wa tuzo BET Awards 2017.
WizKid
Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika katika jiji la (L.A)Los Angeles nchini Marekani katika ukumbi wa Microsoft Theater , Hata hivyo msanii tokea bara la Afrika Wizkid nae ametajwa katika watu watakao weza kushiriki kutoa burudani kwenye Tuzo hizo kubwa huku list hiyo ikiwa na wasanii nguli kama vile Snoop Dogg, Wiz Khalifa, Pusha T, Desiigner, Bryson Tiller, Rae Sremmurd, Jhené Aiko na New Edition.
Future,Bruno na Migos
Katika awamu ya kwanza BET wamewataja pia wasanii kama Migos, Bruno Mars, Future, Trey Songz na Tamar Braxton ndio  watakaoanza kupanda kwenye stage kutoa burudani  katika usiku huo.
Tamasha hilo litakalo fanyika siku nne mfululizo litaoneshwa mubashara kuanzia saa mbili usiku.Msanii Beyoncé na Bruno Mart ndio walioongozwa kutaja katika vipengere tofauti, Huku Beyone akiwania vipengele saba, na Brono Mars akiwania vipengele vitano.Pia wasanii kama Solange, Chance the Rapper na Migos,wakiwa katika vipengere vinne vine.

Comments